8.4 C
New York

Sekta ya Madini Tanzania; bajeti 2026/2027

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

BUNGE la Jamhuru ya Muungano wa Tanzania, limeridhia na kupitisha bajeti ya Wizara ya Madini ya sh bilioni 174.9 kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 ili kuiwezesha Wizara ya Madini kufanikisha ukusanyaji wa maduhuli ya sh trilioni 1.4.

Akiwasilisha Bungeni makadirio ya Mapato na Matumizi Aprili 27, 2026, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema fedha hizo zitawezesha kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake, huku zikilenga kuendeleza kasi ya ukuaji wa sekta ya madini kwa kufanya tafiti za jiosayansi nchini.

Akifafanua mgawanyo wa Bajeti hiyo, Waziri Mavunde amesema kiasi cha sh bilioni 71.5 sawa na asilimia 40.9 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, wakati sh bilioni 103.5 sawa na asilimia 59.1 zikiwa ni matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo, sh bilioni 27.4 ni mishahara ya watumishi na sh bilioni 76.1 ni matumizi mengineyo ya Wizara na taasisi zake.

Kuhusu mwenendo wa Sekta, Waziri  Mavunde amefanunua kuwa,  mchango wa Sekta ya Madini katika kuchangia katika  Pato la Taifa umeendelea kuimarika, ukiongezeka kutoka asilimia 9.1 mwaka 2023 hadi asilimia 10.1 mwaka 2024, na kufikia wastani wa asilimia 11.9 mwaka 2025.

Aidha, Waziri Mavunde ameongeza kuwa ukusanyaji wa maduhuli umeongezeka kwa kiwango kikubwa, kutoka sh bilioni 753.2 mwaka 2023/2024 hadi sh trilioni 1.07 mwaka 2024/2025. Kwa kipindi cha miezi tisa ya mwaka 2025/2026 (Julai hadi Machi), tayari sh trilioni 1.03 sawa na asilimia 114.9 ya lengo lililopangwa.

Katika kuimarisha biashara ya madini, Waziri Mavunde ameeleza kuwa,  idadi ya masoko imeongezeka kutoka 43 hadi 44, huku vituo vya ununuzi vikiongezeka kutoka 114 hadi 118, hatua inayolenga kuongeza uwazi na ushindani wa bei kwa wachimbaji.

Ametaja vipaumbele vya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 kuwa ni kuimarisha mchango wa sekta katika uchumi, kuendeleza mnyororo wa thamani madini muhimu na ya kimkakati, pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika uongezaji thamani.

Vipaumbele vingine ni kuimarisha uendeshaji wa minada na maonesho ya madini ya vito, kuongeza uwekezaji katika tafiti za kina za madini, kurasimisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo, ikiwa pamoja na kuzijengea uwezo taasisi zilizo chini ya Wizara ili kuongeza tija na ufanisi.

Zaidi angalia infographic yetu kwa urahisi zaidi.

Je ungependa kuandaliwa Infographic kwa ajili ya matumizi yako binafsi au kiofisi, wasiliana nasi 0767580313

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img