TEXAS, Marekani
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina, aliweka wazi nia yake ya kuondoka Atletico muda mfupi baada ya kuiongoza Argentina kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Austria.
“Jambo zuri zaidi kwa kila mchezaji ni uhamisho. Sidhani kama huu ni wakati sahihi kuzungumzia hilo lakini siwezi kuficha,” amesema.
Mapema mwezi huu, Real Madrid ilisema Atletico imekataa ofa yake ya euro milioni 150 kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.
Ikumbukwe, ofa hiyo ilikuwa sehemu ya ahadi za Rais Florentino Perez wakati wa kampeni za Uchaguzi wa mwaka huu.


