TORONTO, Canada
SUPASTAA wa timu ya soka ya Taifa ya Brazil, Neymar, ametabiri watakutana na Hispania katika mchezo wa fainali msimu huu wa Kombe la Dunia.
Brazil inasubiri kumalizana na Scotland baada ya kushinda na kutoa sare katika mechi mbili zilizopita.
Neymar yuko kikosini baada ya kuwa nje tangu Oktoba, 2023, lakini hajacheza mchezo wowote msimu huu wa michuano hiyo.
Hata hivyo, nyota huyo wa zamani wa Barcelona na PSG ameshapona majeraha na kuanza mazoezi, hivyo anaweza kuivaa Scotland kesho Juni 24, 2026.
Neymar ameitaja Hispania na kuipotezea Argentina, ambayo nahodha wake, Lionel Messi, ameshafunga mabao matano katika mechi mbili.


