Na mwandishi wetu, Gazetini
YANGA imetangaza viingilio vya uwanjani katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam, huku bei ya chini ikiwa Sh 5,000.
Mechi hiyo itachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, zikiwa ni siku chache tu tangu Yanga ilipofungwa na Azam mabao 3-2.
Huo ulikuwa ni mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA lakini kesho Juni 24, 2026 ni dakika 90 za kutaka na shoka za Ligi Kuu Bara.
Mbali ya kiingilio cha sh 5,000 kwa jukwaa la Saa, pia mashabiki watakaokaa Orbit nao watalipa kiasi kama hicho.
Bei kwa jukwaa la Urusi ni Tsh 10,000, wakati Wings ni sh 20,000 na VIP ni Ts 30,000.


