ISLAMABAD, Pakistan
MWANAHARAKATI wa haki za binadamu nchini Pakistan, Mahrang Baloch, amehukumiwa kifungo cha maisha.
Baloch ameangukiwa na hukumu hiyo katika mashitaka ya ugaidi na kusababisha kifo cha mwanajeshi katika maandamano ya mwaka 2024.
Akishitakiwa sambamba na mwanaharakati mwenzake, Sibghatullah, wakitajwa kuchochea maandamano yaliyosababisha kifo cha Shabbir Ahmed.
Mwanajeshi huyo aliuawa baada ya waandamanaji takribani 40 kuvamia gari la jeshi na kuwashambulia.
Mbali na adhabu hiyo ya kifungo, pia Baloch na Sibghatullah wametozwa faini ya Pauni 543.


