LUSAKA, Zambia
UKIWA ni mwaka mmoja tu tangu kifo cha Rais Edgar Lungu, familia yake imeshinda kesi baada ya Mahakama kuamuru ipewe mwili kwa ajili ya maziko.
Hilo lilikuwa ni ombi la familia, tofauti na Serikali ya Zambia ilivyotaka azikwe kwa heshima, kando na viongozi wengine waliotangulia.
Hivyo basi, kinachosubiriwa ni kuona kama Serikali ya Zambia itachukua hatua nyingine, kwa maana ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa sasa ulioipa ushindi familia ya kiongozi huyo.
Familia imeendelea kutaka mpendwa wao asizikwe na Serikali, huku zikiwapo taarifa kuwa ulikuwa ni msimamo wa Rais Lungu.
Agosti, 2025, Mahakama nchini Afrika Kusini ilitoa uamuzi wa ushindi kwa Serikali ya Zambia kuuchukua mwili wa mwanasiasa huyo.


