25.8 C
New York

Mabilionea wenye umri mdogo zaidi duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TAKRIBANI nusu ya mabilionea wenye umri mdogo duniani (chini ya miaka 30) walipata utajiri huo kupitia biashara walizorithi kutoka katika familia zao.

Kwa mujibu wa Jarida maarufu la Forbes, Ujerumani na Italia ndizo nchi zinazoongoza kwa kuwa na mabilionea wenye umri mdogo zaidi.

Forbes inaeleza kuwa sehemu kubwa ya matajiri hao ni wamiliki wa kampuni za teknolojia, ikiwamo hii ya akili-unde, yaani ‘artificial intelligence’ (AI).

Katika orodha hiyo, kinara ni Clemente Del Vecchio wa Italia, ambaye licha ya umri wake wa miaka 21, ana utajiri wa Dola za Marekani bilioni 6.8. Ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EssilorLuxottica inayojihuisha na utengenezaji wa vifaa vya matibabu ya macho, yakiwamo mawani, inayomilikiwa na familia yake.

Ndugu yake, Luca Del Vecchio, ambaye pia ni bosi wa Kampuni ya hiyo ya EssilorLuxottica, anashika nafasi ya pili, ambapo umri wake ni miaka 24 na ana utajiri wa Dola bilioni 6.8.

Nafasi ya tatu ni ya Johannes von Baumbach wa Ujerumani. Akiwa na umri wa miaka 20 tu, ni bosi katika Kampuni ya utengenezaji wa dawa za binadamu ya Boehringer Ingelheim inayomilikiwa na familia yao. Utajiri wake ni Dola bilioni 6.6.

Anafuatiwa na ndugu zake watatu – Franz (24), Katharina (26) na Maximilian (28), ambao pia ni mabosi wa Boehringer Ingelheim, kila mmoja akiwa na utajiri kama huo (Dola bilioni 6.6).

Wengine ni Kevin David Lehmann, raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 23, ambaye ana utajiri wa Dola bilioni 4.9 kupitia Kampuni ya familia iitwayo Drogerie Markt. Mbali ya vifaa-tiba, pia inajihusisha na utengenezaji wa vipodozi.

Related articles

Recent articles