28.6 C
New York

Barcelona yaambiwa imchukue Osimhen

Published:

CATALUNYA, Hispania

NI ushauri wa mkongwe Andres Iniesta, akiitaka klabu yake ya zamani ya Barcelona kumsajili straika wa Galatasaray, Victor Osimhen.

Kwa mujibu wa Iniesta, nyota huyo wa kimataifa wa Nigeria ni mtu sahihi wa kuvaa viatu vya Robert Lewandowski aliyeondoka Camp Nou na kutua Chicago Fire ya Marekani.

Wakati huu wa dirisha kubwa la usajili wa kiangazi, Barcelona imekuwa ikihusishwa pia na straika wa Atletico Madrid, Julian Alvarez.

“Sidhani kama Atletico Madrid watamwachia Julian Alvarez. Ningependekeza asajiliwe Victor Osimhen,” amesema Iniesta.

Akimzungumzia Osimhen na sifa zake, lejendari huyo wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania alisema: “Ni mfungaji nzuri na ni miongoni mwa walio bora kuziba pengo la Robert Lewandowski.”

Related articles

Recent articles