28.7 C
New York

A-Z ya mashuti, asisti, mabao Kombe la Dunia 2026

Published:

BOSTON, Marekani

FAINALI za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026) zilizochezwa kwa siku 39, kwenye viwanja 16, zikishirikisha wachezaji 1,039 kutoka timu 48, zilishuhudia mabao 308 yakifungwa katika mechi 104.

Je, ni nani aliyeongoza kwa mabao, asisti? Ni timu zipo zilizofunga na kuruhusu mabao mengi? Makala fupi haya yanachambua.

MABAO YA KUFUNGA

Kylian Mbappe wa Ufaransa ndiye aliyeongoza kwa mabao 10, akifuatiwa na Lionel Messi (8), Jude Bellingham na Erling Haaland (7), na Ousmane Dembele na Harry Kane (6).

Wakati huo huo, timu za taifa zilizoongoza kwa kufunga mabao ni England na Ufaransa, kila moja ikiwa na 20 kwenye mashindano hayo.

ASISTI HIZI HAPA

Kinara wa pasi za mabao (asisti) ni Michael Olise wa Ufaransa akiwa na saba, akifuatiwa na Martin Odegaard, Mbappe, Brahim Diaz, Bruno Guimaraes, na Messi, kila moja akiwa na nne.

Timu za taifa zilizoongoza kwa idadi kubwa ya asisti ni Ufaransa (18), England (14), Argentina (12), Hispania na Ubelgiji (10).

MASHUTI, UMILIKI WA MPIRA

Ufaransa imememaliza msimu huu wa Kombe la Dunia ikiwa kinara wa mashuti, ikipiga 139, huku 59 yakilenga lango. Umiliki wa mpira katika mechi zake ni asilimia 51.

Katika nafasi ya pili ni England; mashuti 118 (52 yalilenga lango) na wastani wa umiliki wa mpira ni asilimia 50.

MAKIPA WALIOOKOA MABAO MENGI

Kinara ni Orlando Gill wa Paraguay (28), akifuatiwa na Eloy Room (Curacao, 21), Emiliano Martinez (Argentina, 20), Gregor Kobel (Uswis, 20), na Diogo Costa (Ureno, 20).

Wengine ni Jordan Pickford (England, 19), Yassine Bounou (Morocco, 19), Vozinha (Cape Verde, 18), Zion Suzuki (Japan, 17), na Mohammed Al Owais (Saudi Arabia, 17).

Hata hivyo, Unai Simon wa Hispania ndiye aliyecheza mechi nyingi (7) bila kuruhusu bao, hivyo kutwaa tuzo ya Kipa Bora wa mashindano.

MABAO YA KUJIFUNGA

Katika fainali za mwaka huu, timu 10 zilijifunga bao moja kila moja, huku Qatar na Misri zikitia fora kwa kujifunga mara mbili.

Timu zilizoruhusu mabao mengi ni Iraq, Tunisia na England, kila moja nyavu zake zikitikiswa mara 12, zikifuatiwa na
Uzbekistan na Norway (11).

New Zealand, Sweden, Ufaransa na Qatar kila moja imepitisha mabao 10, huku Curacao, Senegal, Algeria na Austria zikifuata kwa mabao tisa.

KADI ZA NJANO

Argentina iliongoza kwa kasi za njano (15), Misri ikishika nafasi ya pili (12), ikifuatiwa na Canada (11), Paraguay (9),
Brazil, England, Uswis, Colombia na Ecuador (8), Curacao, Ureno, Marekani, Haiti, Morocco, na Bosnia (7).

Wakati huo huo, Qatar na Afrika Kusini ndizo zilizoongoza kwa kadi nyekundu, kila moja ikikutana nayo mara mbili.

Related articles

Recent articles