20.5 C
New York

Motsepe: Infantino ni rafiki wa kweli wa Afrika

Published:

CAIRO, Misri

RAIS wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amempongeza Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, akimtaja kuwa kiongozi mwaminifu wa mchezo wa soka na rafiki wa kweli wa bara la Afrika.

Akizungumza Julai 22, 2026 mjini Cairo, Misri, Motsepe amemesema chini ya uongozi wa Infantino, FIFA imeendelea kuonyesha dhamira ya kuendeleza soka la Afrika kupitia kuongeza fursa za ushiriki katika mashindano ya kimataifa, kuimarisha uwekezaji wa miundombinu ya soka na kukuza vipaji vya wachezaji.

“Gianni Infantino ni msimamizi mwaminifu wa mchezo wa kandanda na rafiki wa Afrika. Ameonyesha kwa vitendo kujitoa kwake katika maendeleo ya soka letu na kuhakikisha bara la Afrika linapata nafasi stahiki katika mchezo wa kimataifa,” amesema Motsepe.

Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya CAF na FIFA umechangia kuimarika kwa maendeleo ya soka barani Afrika, huku akisisitiza kuwa viongozi hao wataendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuinua kiwango cha mchezo huo na kuongeza ushindani wa timu za Afrika katika mashindano ya kimataifa.

Related articles

Recent articles