CARDIFF, Wales
WALES imekuwa nchi ya kwanza kutangaza kutokumuunga mkono Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, katika mpango wake wa kuwania tena kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani (2027).
Hilo ni pigo jingine kwa Infantino, ambaye hivi karibuni alikosolewa vikali kwa mpango wake wake wa kuuza hisa za michuano yote ya FIFA.
Ni kutokana na ukosoelewaji mkubwa, Katibu huyo wa zamani wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) alilazimika kujitokeza na kutangaza kuwa ameachana na mpango huo.
Kama itakumbukwa, UEFA ilienda mbali zaidi na kudai kuwa lingesusia fainali za Kombe la Dunia endapo Infantino angeng’ang’ania mpango wake huo.
Katika taarifa yake, Chama cha Soka cha Wales (FAW) kimeeleza kuwa hakivutiwi na utendaji kazi wa hivi karibuni wa kiongozi huyo, hivyo hakitokuwa upande wake ifikapo mwaka 2027.


