27.2 C
New York

Norway kumshitaki Trump kisa Kombe la Dunia

Published:

OSLO, Norway

SHIRIKISHO la Soka la Norway (NFF) limetangaza nia yake ya kumshitaki Rais Donald Trump kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Norway wanapeleka barua yao kwa FIFA wakilalamikia Rais Trump kuingilia adhabu ya kadi nyekundu ya mshambuliaji wa timu ya soka ya Taifa ya Marekani, Folarin Balogun, wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026).

Balogun alipaswa kuikosa mechi yao ya hatua ya 16 Bora dhidi ya Ubelgiji kutokana na kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa nyuma yake (dhidi ya Bosnia).

Hata hivyo, ilikuja kuelezwa kuwa Trump aliwasiliana kimyakimya na Rais wa FIFA, Infantino, na ndipo Balogun alipoingia kuivaa Ubelgiji.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Norway kumkalia kooni Rais Trump kwani waliwahi kulalamikia kitendo cha FIFA kumpa tuzo ya Amani kiongozi huyo, wakisema soka halipaswi kuchanganywa na siasa.

Related articles

Recent articles