21.6 C
New York

Vijana wa Liberia na urahibu wa bangi

Published:

MONROVIA, Liberia

KATIKA mitaa ya Mji Mkuu, Monrovia, utumizi wa dawa za kulevya aina ya bangi si jambo linalohitaji utafiti mkubwa kulibaini, na badala yake linaonekana wazi, hasa kwa vijana.

Kwa wazazi, uvutaji wa ‘kush’ umesababisha vijana wao wengi kuacha shule, kukimbia nyumbani, na kujiingiza katika vitendo vya uhalifu, ikiwamo wizi.

Thomas Wesseh, licha ya jitihada za kuwasaidia polisi kuvifahamu vijiwe vya wavutaji, mtoto wake aliingia kwenye shimo hilo na kuacha chuo akiwa mwaka wa pili.

Mbaya zaidi, vijana wanapoingia katika janga hilo, hupotea moja kwa moja na kushindwa kurudi katika maisha yao ya zamani, kwa mujibu wa wazazi waliohoajiwa na kituo cha televisheni cha Al Jazeera.

Mmoja ya wazazi hao, Paye, ameiambia Al Jazeera kuwa kijana wake alianza kutumia kilevi hicho mwaka 2018, wakati huo akiwa mwanafunzi wa sekondari.

“Nililipa mara mbili gharama za kumpeleka kituo cha tiba ya kuondokana na urahibu. Mara zote hizo nilitoa Dola 80, kilo 25 za mchele, na fedha za kujikimu,” anasema Paye.

Hata hivyo, licha ya jitihada hizo, achilia mbali gharama, Paye alivunjika moyo kuona kijana wake anarudia matumizi ya bangi kila alipotoka kituoni. “Inatuulia vijana wetu. Moyo wangu unavuja damu,” anasema.

UKUBWA WA TATIZO

Ripoti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya Liberia (LDEA) inaonesha kuwa watu 1,167 walikamatwa (wakisafirisha dawa za kulevya) kuanzia Septemba, 2025, hadi Juni, 2026.

Hata hiyo, kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja, ni mashitaka nane pekee yaliyofikishwa mahakamani, sawa na shitaka moja katika kila watu 146 waliokamatwa.

Takwimu hizo zinaibua swali; je, mamlaka zinawafikia na kuwatia nguvuni wahusika wa moja kwa moja wa biashara ya dawa za kulevya?

Juni 8, 2026, polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert mjini Harbel, Kusini-Mashariki mwa Monrovia, walikamata kilo 237.6 za cocaine zenye thamani ya Dola milioni 19.2.

Wiki chache baadaye, polisi walivamia jengo moja mjini Duazon na kubaini tani nne za cocaine, kiwango kikubwa zaidi cha dawa za kulevya kuwahi kukamatwa na Serikali nchini humo.

Aidha, takwimu za LDEA zinaonesha kuwa kiwango cha bangi zilizokamatwa kimeongezeka mara mbili, kutoka kilo 80.15 mwaka 2025 hadi kilo 166.88 mwaka 2026.

Kwa mujibu wa Mamlaka hiyo, asilimia 38 ya waliokamatwa ni raia wa kigeni kutoka katika mataifa ya Ivory Coast, Guinea, Nigeria na Sierra Leone.

UMASIKINI, MIGOGORO YA FAMILIA

Abraham Jackson, ni miongoni mwa vijana wanaoishi mitaani baada ya kupotea katika matumizi ya bangi. Alianza kuvuta akiwa na umri wa miaka 16 na sasa ana miaka 26.

Kwanini alijiingiza humo na kushindwa kumaliza elimu ya sekondari? Anasema: “Tangu mama alipofariki, baba alinitelekeza. Sikuwa na mtu wa kuniangalia.”

Related articles

Recent articles