26.6 C
New York

Awamu ya I uvutaji nyaya Chalinze-Dodoma yakamilika

Published:

Na mandishi wetu, Gazetini

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema Mkandarasi  amekamilisha  kwa mafanikio awamu ya kwanza ya kazi za uvutaji wa nyaya katika eneo la Mkambarani, Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni sehemu ya hatua za mwisho za utekelezaji wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 5, 2026 katika eneo la Mkambarani, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Irene Gowelle, amesema zoezi hilo, ambalo lilipangwa kufanyika ndani ya siku sita, limekamilika kwa mafanikio na kwa wakati uliopangwa, hatua ambayo imewezesha kurejea kwa huduma ya umeme katika mikoa yote iliyokuwa imeathiriwa na kazi hiyo na kufanya shughuli kuendelea kama kawaida.

Gowelle amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha na kuongeza uwezo wa Gridi ya Taifa, hatua itakayowezesha usafirishaji wa umeme kwa uhakika zaidi katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Aidha amewashukuruwananchi na wateja wa Tanesco kwa uvumilivu, ushirikiano waliouonesha katika kipindi chote cha utekelezaji wa kazi hizo.

 Ameongeza kuwa Tanesco itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo nchini.

“Kazi hii imefanyika kwa mafanikio makubwa na kwa wakati uliopangwa. Tunawashukuru sana wateja wetu kwa uvumilivu wao. Kwa sasa huduma ya umeme imerejea kama kawaida. Hata hivyo, napenda kuwakumbusha kuwa zoezi hili litaendelea kwa awamu ya pili katika maeneo ya Mkonze na Kikombo kuanzia Agosti 11 hadi 14. Tutawatangazia ratiba mapema ili muweze kupanga shughuli zenu kulingana na ratiba ya upatikanaji wa umeme,” amesema Gowelle.

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa Chalinze–Dodoma, Mhandisi Newton Mwakifwamba, amesema awamu ya kwanza ya uvutaji wa nyaya ilitekelezwa katika eneo la Mkambarani, ikihusisha uvutaji wa nyaya juu ya reli ya SGR, juu ya njia za umeme za Msongo wa Kilovolti 220 za Morogoro I na Morogoro II, pamoja na njia ya Msongo wa Kilovolti 132, na kwamba kazi zote zimefanyika kwa ufanisi mkubwa.

Ameeleza kuwa awamu ya pili ya uvutaji wa nyaya itafanyika katika maeneo ya Kikombo na Mkonze Dodoma kuanzia Agosti 11 hadi 14, ambapo shughuli hizo zitafanyika kwa wakati mmoja. Kutokana na hali hiyo, kutakuwa na katizo la umeme kwa muda katika baadhi ya maeneo ili kutoa nafasi ya utekelezaji salama wa kazi hizo.

“Umuhimu wa mradi huu ni mkubwa kwa kuwa utaongeza uwezo wa njia zilizopo za kusafirisha umeme. Mradi huu wa Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma utaimarisha uwezo wa Gridi ya Taifa na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme nchini,” amesisistiza Mwakifwamba.

Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa Kilovolti 400 kutoka Chalinze hadi Dodoma umefikia asilimia 94 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika Agosti 21, 2026. Kukamilika kwake kutaongeza uwezo wa mfumo wa usafirishaji wa umeme nchini na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme yenye ubora na uhakika kwa wananchi.

Aidha, EWURA imewataka wananchi kutoa taarifa endapo watabaini vituo vya mafuta vinavyouza mafuta kwa bei inayozidi bei kikomo au vinavyokiuka masharti ya utoaji wa huduma.

Kushuka kwa bei za mafuta kunatarajiwa kupunguza gharama za usafirishaji na uzalishaji katika baadhi ya sekta za uchumi, hatua inayoweza kuwa na manufaa kwa watumiaji na wafanyabiashara endapo mwenendo huo utaendelea.

Related articles

Recent articles