6.4 C
New York

Visual| Mabilionea 10 walioishika Dunia

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KWA mujibu wa Jarida maarufu la Forbes, mfanyabiashara wa Marekani, Elon Musk, ndiye binadamu mwenye fedha nyingi zaidi duniani. Utajiri wake ni Dola bilioni 714.

Forbes inayaona kasi kubwa mabadiliko makubwa katika nafasi za matajiri duniani, ambapo mmiliki wa kampuni ya Amazonz, Jeff Bezos, alikuwa namba moja miaka mitano tu iliyopita.

Wakati huo, 2020, Bezos alikuwa na utajiri wa Dola bilioni 145 na sasa amezidiwa takribani mara tano na raia mwenzake wa Marekani, Musk.

Musk ambaye mwaka 2020 alikuwa na utajiri wa Dola bilioni 24.6, leo hii ndiye kinara wa ‘mkwanja’ katika uso wa dunia.

Bezos, kwa mujibu wa ripoti ya sasa ya Forbes, anashika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa bilioni 251.4, akizidiwa na mwenzake wa Marekani, Larry Page, anayeshika nafasi ya pili (Dola bilioni 257.7).

Lakini, kati ya matajiri 10 wa dunia, nafasi sita za juu zinashikwa na wafanyabiashara wa Marekani, ambapo wengine ni Larry Ellison wa nafasi ya nne akiwa na bilioni 242.6.

Katika orodha hiyo, anafuatiwa na Sergey Brin mwenye utajiri wa Dola bilioni 237.8 na Marc Zuckerberg (Dola bilioni 226.5).

Aidha, Bernard Arnault wa Ufaransa (Dola bilioni 193.9) na Amancio Ortega wa Hispania ni wafanyabiashara pekee wa nje ya Marekani walioingia kwenye ‘Top 10’, kwa mujibu wa Forbes.

Wamarekani wengine katika orodha hiyo ni Jensen Huang aliye nafasi ya nane (Dola bilioni 162.5) na Warren Buffett aliye nyuma yake (Dola bilioni 147.5).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img