24.8 C
New York

Asali sasa dili Marekani, uzalishaji wapungua

Published:

NEW YORK, Marekani

KUNA uhitaji mkubwa wa asali nchini Marekani baada ya kiwango cha uzalishaji kushika kwa kiwango kikubwa zaidi kuwahi kutokea, kwa mujibu wa Idaa ya Kilimo ya Taifa hilo.

Katika taarifa yake, imeeleza kuwa uzalishaji wa asali umepungua kwa asilimia 14, ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2024.

Kwa mujibu wa Idara ya Kilimo, anguko hilo ni kubwa na la kwanza tangu ilipoanza kukusanya takwimu mwaka 1939.

Wakati huo huo, manunuzi ya mtu mmoja mmoja ya asali yameripotiwa kuongezeka. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za kuanzia Machi, 2024 hadi Machi 2025.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Wamarekani wamenunua asali zenye thamani ya Dola bilioni 1.6, likiwa ni ongezeko la asilimia 10, ikilinganishwa na mwaka 2023-24.

Related articles

Recent articles