25 C
New York

50 Cent, Diddy uadui wao tangu kitambo!

Published:

LOS ANGELES, Marekani

SIO jambo geni kwamba mastaa wa Hip hop nchini Marekani, Curtis Jackson ’50 Cent’ na Sean Combs ‘Diddy’, wamekuwa kwenye uhusiano mbaya kwa muda mrefu.

Cent alikuwa mstari wa mbele kumkashifu Diddy baada ya kuvuja kwa video iliyomuonesha Diddy akimtembezea kichapo aliyekuwa mpenzi wake, Cassie Ventura.

Tangu hapo, Cent hajawahi kuacha kumshambulia Diddy kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Swali la kujiuliza; uadui uliopo sasa kati ya marapa hao wenye mafanikio makubwa kwenye soko la muziki duniani ulianzia wapi? Makala haya yanachambua.

Stori inaanzia Machi, 1997, katika tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa rapa mwenzao, Christopher Wallace, maarufu zaidi kwa jina la ‘The Notorious B.I.G’.

Ripoti zinaeleza kuwa siku ya tukio, B.I.G. na washikaji zake, akiwamo Diddy aliyekuwa kwenye gari tofauti, walikuwa kwenye msafara mmoja mjini Los Angeles.

Baada ya watu wasiojulikana kumpiga risasi B.I.G. na kumuua, Diddy aliingia kwenye skendo, akihusishwa kusuka mpango wa kumtoa uhai rapa mwenzake huyo.

Sasa, Cent ni miongoni mwa walioamini hilo kuwa na alithibitisha kupitia wimbo wake maarufu wa ‘The Bomb’ alioachia mwaka 2006.

Katika ngoma hiyo, inasikika milio ya risasi na Cent anadai kuwa Diddy anamfahamu vizuri mtu aliyempiga risasi B.I.G.

Kama hiyo haitoshi, Cent amewahi kusema Diddy pia ndiye aliyemuua rapa mwingine maarufu, Tupac Shakur, ambaye alipigwa risasi miezi michache tu kabla ya B.I.G. kuuawa.

Kwa upande wake, Diddy amekuwa akiyaita kuwa ni upumbavu madai yote ya kuhusishwa na vifo vya malejendari hao wa Hip hop.

Pia, licha ya kashfa nyingi kutoka kwa Cent, Diddy, ambaye kwa sasa yuko gerezani kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono, aliendelea kusema hana ‘bifu’ na Cent na anaamini rapa mwenzake huyo anampenda.

Akihojiwa kupitia kipindi cha televisheni cha ‘The Breakfast Club’ mwaka 2018, Diddy alisema: “Huwa sichukii anachosema. Najua yuko tofauti lakini siwezi kusema chochote kibaya kuhusu yeye.”

Related articles

Recent articles