Na mwandishi wetu, Gazetini
KWA zaidi ya miongo miwili sasa, kampuni ya PMM Estates (2001) Limited imeendelea kujijengea heshima kama moja ya taasisi muhimu katika sekta ya bandari kavu (Inland Container Depot – ICD), usafirishaji na uhifadhi wa mizigo nchini Tanzania.
Kampuni hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2001 na kusajiliwa chini ya sheria za kampuni za Tanzania, ikiwa na makao yake makuu jijini Dar es Salaam, eneo lenye umuhimu mkubwa wa kibiashara kutokana na ukaribu wake na Bandari ya Dar es Salaam na miundombinu mikuu ya usafiri.
Awali, PMM Estates ilianza kama kampuni ya usimamizi wa mali (estate management), lakini kutokana na ukuaji wa mahitaji ya huduma za usafirishaji na uhifadhi wa makasha, uongozi wa kampuni chini ya mwasisi wake, Dk Judith Sipendi, uliamua kubadili mwelekeo wa biashara na kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya ICD na logistics. Hatua hiyo iliifanya kampuni kujikita zaidi katika kusimamia, kuhifadhi na kusafirisha makasha ya mizigo yanayoingia na kutoka bandarini.
Kupitia uwekezaji katika ardhi, vifaa vya kisasa na rasilimali watu, PMM Estates ilifanikiwa kupata leseni rasmi ya uendeshaji wa bandari kavu na kuanza kufanya kazi kwa karibu na taasisi kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na wadau wengine wa bandari.
Kwa sasa, kampuni hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo uhifadhi wa makasha, ushughulikiaji wa mizigo, usafirishaji wa ndani ya nchi, pamoja na ulinzi na usimamizi wa mizigo safarini. Huduma hizi zimekuwa zikitekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya usalama na ufanisi.
Katika upande wa ufanisi (yanufanisi), PMM Estates imejipambanua kwa:
Kupunguza msongamano wa mizigo bandarini kwa kuhifadhi makasha nje ya bandari,
Kuharakisha mnyororo wa usafirishaji (logistics chain) kwa wateja wake,
Kuimarisha usalama wa mizigo na kupunguza hasara,
Kuongeza tija kupitia matumizi ya rasilimali watu wenye uzoefu na vifaa vinavyoendana na mahitaji ya soko.
Zaidi ya mchango wake katika biashara, PMM Estates pia imekuwa chanzo cha ajira kwa Watanzania wengi na mdau muhimu katika kukuza uchumi wa ndani kupitia ukusanyaji wa kodi na ushirikiano na wafanyabiashara na makampuni mengine.
Uongozi wa kampuni unaongozwa na wataalamu wenye uzoefu katika sekta ya usafirishaji, biashara na usimamizi, hali inayochangia maamuzi ya kimkakati na ukuaji endelevu wa taasisi hiyo.
Kwa kuzingatia mwelekeo wa Serikali wa kuimarisha Bandari ya Dar es Salaam na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji kikanda, PMM Estates (2001) Ltd inaendelea kujipanga kupanua shughuli zake, kuongeza ufanisi wa huduma na kuendelea kuwa mshirika muhimu katika safari ya maendeleo ya sekta ya bandari na logistics nchini.


