Na mwandishi wetu, Gazetini
NI kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2022 na kuchapishwa mwaka 2024, ukionesha kuwa Denmark, Norway, Finland, Sweden na Iceland ndiyo mataifa yanayoongoza kwa watu wake kuaminiana.
Wakati huo huo, China yenye asilimia 63 imekuwa Taifa pekee la barani Asia lililoingia kwenye nafasi 10 za juu, kwa mujibu wa utafiti huo wa Our World in Data.
Utafiti huo ulihusisha nchi 90 duniani. Watafiti waliwafikia na kuwahoji watu 1,000 hadi 15,000 katika kila nchi, ambapo Denmark ilionekana kuwa na kiwango kikubwa (78%) cha watu wake kuaminiana kwenye masuala mbalimbali.

Kwa upande mwingine, Norway na Finland zinafuata katika nafasi ya pili na ya tatu kwa asilimia 72 na 68, zikifuatiwa na China na Sweden (63%), Iceland (62%) na Uswis (59%), Uholanzi na New Zealand (57%) na Austria (50%).
Hata hivyo, kiwango cha watu wake kuaminiana kimeonekana kuwa kidogo kwa mataifa ya Canada (47%), Uingereza (43%), Ujerumani (42%), Marekani (37%), Ufaransa (26%) na Italia (27%).
Pia, mataifa mengine yaliyoonekana kufanya vibaya kwenye suala la raia wake kuaminiana ni Iraq (11%), Lebanon (10%), Misri (7%), Peru na Nicaragua (4%), Colombia (5%) na Ecuador (6%).


