26 C
New York

Jembe jipya Arsenal lachimba mkwara

Published:

LONDON, Uingereza

KIUNGO wa kimataifa wa Brazil, Bruno Guimaraes, amesema amewaahidi mashabiki wa Arsenal kuwa ataendeleza moto aliokuwa nao Newcastle United.

Arsenal walikamilisha usajili wake wikiendi iliyopita baada ya miezi mingi ya kuifukuzia saini ya nyota huyo.

Akizungumza baada ya kukamilsha dili hilo, Guimaraes amesema ndoto yake ni kucheza kwa kiwango bora na kuisadia Arsenal kutwaa mataji.

“Nitajitahidi kuisaidia timu, nina uwezo mkubwa nikiwa na mpira, utulivu na wakati mwingine naweza kufunga mabao na kumfurahisha kila mmoja,” amesema.

Guimaraes kutua Emirates ni pigo kubwa kwa klabu nyingi za Ulaya, ikiwamo Manchester City, ambazo pia zilijaribu kuiwania saini yake.

Related articles

Recent articles