26 C
New York

FIFA yalaani mpango wa kumng’oa Infantino

Published:

NYON, Uswis

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limelaani mpango wowote unaolenga kumng’oa kwenye kiti Rais wake, Gianni Infantino.

Infantino anakabiliwa na shinikizo la kutakiwa kujiuzulu baada ya mpango wake wa kuuza hisa za mashindano yote ya FIFA kukataliwa.

Katika taarifa yake, FIFA imedai kubaini njama za baadhi ya vyama na mashirikisho ya soka kuichafua Taasisi hiyo na Rais wake.

“… Rais wa FIFA alichaguliwa kwa misingi ya kidemokrasia na vyama wanachama na ataendelea kushikilia mamlaka hayo,” imesomeka sehemu ya taarifa ya Shirikisho hilo.

Wakati huo huo, FIFA imeeleza kuwa kwa sasa inajielekeza katika mikakati yake ya kuimarisha maendeleo ya soka na si kujihusisha na propaganda zinazoendelea.

Related articles

Recent articles