26 C
New York

Maresca kuchagua nahodha mpya Man City

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA wa Manchester City, Enzo Maresca, yuko mbioni kutangaza nahodha mpya wa kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa 2026-27.

Man City inahitaji nahodha wa kuvaa kitambaa cha Bernardo Silva ambaye ameondoka klabuni hapo majira haya ya kiangazi na kutua Real Madrid.

Wakati huo huo, Man City wanaweza pia kumpoteza kiungo wake raia wa Hispania, Rodri, ambaye anawindwa na Barcelona.

Kwa kuwa wakongwe hao hawatokuwepo, Ruben Dias anapewa nafasi kubwa ya kukabidhiwa mikoba ya unahodha pale Etihad.

Katika hatua nyingine, jina la mpachikaji mabao hatari raia wa Norway, Erling Haaland, nalo limeanza kuhusishwa na majukumu hayo.

Related articles

Recent articles