6.4 C
New York

Mastaa wa muziki Nigeria tishio pesa za shoo

Published:

LAGOS, Nigeria

KAMA ilivyo duniani kote, tasnia ya burudani, likiwamo soko la muziki, imeendelea kuwa chanzo kikubwa cha utajiri kwa mastaa nchini Nigeria. Kwa wanamuziki, kufanya shoo ni moja ya vyanzo vya mapato, ingawa pia wamekuwa wakivuna fedha nyingi kupitia mauzo ya kazi zao.

Davido, ambaye amekuwa na ushawishi mkubwa kwa wapenzi wa muziki wa Afrobeat, huingiza Dola 600,000 (zaidi ya Sh bil. 1.4 za Tanzania) kila anapopanda jukwaani kutumbuiza. Hata hivyo, zipo taarifa kuwa mwimbaji huyo huchota hadi Dola milioni 10 (zaidi ya Sh bil. 24 za Tanzania) anapoalikwa kutumbuiza katika sherehe za mabilionea nchini Nigeria.

Nje ya shoo, pia kuna gharama za kufanya kolabo. Ikielezwa kuwa huwa analipwa hadi Dola 400,000 kwa kushiriki wimbo wa msanii mwingine, achilia mbali Dola 800,000 endapo atatokea kwenye video.

Huyo ni Davido. Kwa upande wa mpinzani wake mkubwa, Wizkid, yeye huhitaji hadi Dola milioni 2 kumpata kwenye shoo. Staa mwingine anayefanya vizuri kwenye soko la muziki wa Afrobeats, Burna Boy, analipwa Dola milioni moja kupanda jukwaani kwenye shoo za kimataifa.

Hata hivyo, nje ya fedha hizo, kuna makubaliano mengine ambayo promota anapaswa kuyafikia na kuyatekeleza. Miongoni mwao ni usafiri wa ndege binafsi yenye uwezo wa kubeba watu 13.

Pia, Burna Boy atahitaji promota ampatie magari ya kifahari yasiyopungua 15, ulinzi wa uhakika, na hoteli ya nyota tano yenye vyumba 60 kwa ajili ya timu yake. Inaelezwa kuwa hata promota akimudu kulipa ada ya shoo, Burna Boy hatohudhuria endapo vigezo vingine havitozingatiwa. Aliwahi kukataa shoo ya Dola milioni 5 kwa kuwa tu baadhi ya mahitaji yake mengine hayakufikiwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img