6.4 C
New York

Mataifa yanayoongoza kwa madeni duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
DENI la Dunia limefikia Dola za Marekani trilioni 110.9 lakini zipo nchi zinazooneka kuwa kinara wa kukopa, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika ripoti yake ya Oktoba, mwaka huu.
Takwimu hizo za IMF zimetokana na uwiano uliopo kati ya deni la Serikali na Pato la Taifa husika (GDP), huku Marekani, China, Japan, Uingereza na Ufaransa zikiongoza kwa kukopa.
Kwa mujibu wa ripoti mpya hiyo ya IMF, nchi tano hizo, licha ya kufanya vizuri kiuchumi duniani kutokana na maendeleo makubwa ya viwanda, zimetengeneza deni la jumla ya Dola trilioni 74.8
Marekani ni kinara ikiwa na deni la Dola trilioni 38.27, ikifuatiwa na China (Dola trilioni 18.68), Japan (Dola trilioni 9.83), mataifa hayo yakitengeneza asilimia 60 ya deni lote la Dunia.
Kwa upande mwingine, wakati deni la Marekani likiwa linapanda kwa asilimia 8.4 kila mwaka, China limekuwa likipanda zaidi (13.6%).
Japan, licha ya kuingia kwenye orodha hiyo, ripoti ya IMF inaonesha kuwa deni lake limepungua kwa asilimia 2, sawa na Dola bilioni 200.
Mataifa mengine kwenye orodha ya madeni ya IMF ni Uingereza (Dola trilioni 4.09), Ufaransa (Dola trilioni 3.92), Italia (Dola trilioni 3.48), India (Dola trilioni 3.36), Ujerumani (Dola trilioni 3.26), Canada (Dola trilioni 2.60), na Brazil (Dola trilioni 2.06).
Serikali ya Hispania nayo imo kwenye listi hiyo ikiwa na deni la Dola trilioni 1.90, ikifuatiwa na Mexico (Dola trilioni 1.10), Singapore (Dola trilioni 1.01), Korea Kusini (Dola trilioni 0.99), na Australia (Dola trilioni 0.93).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img