13.1 C
New York

Chart| Kilimanjaro kinara kwa idadi ya wazee Tanzania

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

KULINGANA na takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imebaini kuwa mkoa wa Kilimanjaro unaongoza nchini kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea, wakifikia asilimia 10.4 ya wakazi wake.

Mikoa mingine inayofuata kwa idadi ya wazee ni Mtwara yenye asilimia 9.1, Lindi 8.6%, Tanga 7.6% na Njombe 7.3%. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa baadhi ya mikoa nchini inajulikana kwa mazingira yanayochangia maisha marefu, ikiwemo lishe bora, mshikamano wa kijamii na hali nzuri ya kijiografia.

Wazee wanachukuliwa kuwa hazina ya busara na kumbukumbu ya historia ya taifa letu. Ni jukumu la jamii na Serikali kuhakikisha wanapata huduma bora za afya, heshima, ulinzi wa haki zao na mshikamano wa kijamii. Aidha, kuwahimiza wazee kushiriki katika shughuli za kijamii kunachangia ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.

Hii takwimu pia inatoa mwongozo kwa Serikali na mashirika ya kijamii kupanga mipango endelevu ya kuwahudumia wazee, hasa katika mikoa yenye idadi kubwa ya wazee. Zaidi ya hayo, uchunguzi zaidi unaweza kusaidia kubaini sababu zinazochangia maisha marefu ili kuweza kunufaisha mikoa mingine nchini. Zaidi angalia #chart yetu hapo juu kwa ufahamu wa kina.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img