JERUSALEM, Israel
WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema wamkataa ombi la Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mgogoro wa Gaza.
Kwa mujibu wa Netanyahu, hawakubaliani na ombi la Trump kutaka Israel iondoshe wanajeshi wake katika Ukanda huo.
Katika maelezo yake, Netanyahu amesisitiza kuwa wanajeshi wa Israel wataondoka endapo watajiridhisha kwamba Kundi la Hamas limetokomezwa.
Hamas ni kundi linalohusishwa na ugaidi na linajitaja kupigania na kulinda masilahi ya raia wa Palestina dhidi ya uhalifu wa Israel.
Licha ya kusema wamekataa ombi la Trump, Netanyahu amesisitiza kuwa Israel haitojitoa katika meza ya mazungumzo na Marekani katika kusaka suluhu ya mgogoro huo wa Gaza.


