24.5 C
New York

Arsenal yasaka mrithi wa Vinicius Jr

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL imeangukia pua katika mbio zake za kuiwania saini ya Vinicius Jr baada ya Mbrazil huyo kusaini mkataba mpya wa miaka sita katika klabu yake ya Real Madrid.

Arsenal walishafikia hatua nzuri kwa Vinicius mwenye umri wa miaka 26 lakini winga huyo alibadili uamuzi na kubaki Santiago Bernabeu.

Hivyo, sasa inaelekeza nguvu kwa mshambuliaji wa Atletico Madrid, Julian Alvarez, ambaye pia anawaniwa na mabingwa wa La Liga, Barcelona.

Washika Bunduki wanapaswa si tu kukomaana na Barcelona, bali pia kuwa na ushawishi mkubwa mbele ya mabosi wa Atletico walioweka wazi kuwa hawana mpango wa kumwachia Muargentina huyo.

Kama si Alvarez, mchezaji mwingine anayeweza kusajiliwa na Arsenal kuziba pengo la Vinicius Jr ni staa wa PSG raia wa Ufaransa, Bradley Barcola.

Mkataba wake na matajiri hao wa Ligue 1 utafikia ukomo mwaka 2028 na tayari amegoma kuongeza mwingine, akiweka wazi nia yake ya kuondoka.

Liverpool wako mstari wa mbele kuiwania saini yake na vyanzo vya habari nchini Uingereza vinaeleza kuwa wamepanga kupeleka ofa yao ya euro milioni 115.

Kwa upande wao, PSG wako tayari kumfungulia mlango wa kutokea lakini wanataka kufanya biashara na klabu itakayoweka mezani kitita cha euro milioni 150.

Katika hatua nyingine, Washika Bunduki wa London wanamtolea macho winga wa Everton, Iliman Ndiaye. Msenegal huyo alifunga mabao sita na kutoa ‘asisti’ tatu msimu uliopita (2025-26).

Mkataba wake na Everton utamalizika mwaka 2029, hivyo klabu hiyo inaweza kuvutiwa na mpango wa kumuuza kipindi hiki ili kupata fedha nyingi.

Related articles

Recent articles