24.5 C
New York

Lwandamina apigiwa debe ajira Chipolopolo

Published:

HARARE, Zimbabwe

KIUNGO wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’, Gift Kampamba, anaamini George Lwandamina anastahili kuajiriwa moja kwa moja kukinoa kikosi hicho.

‎Lwandamina aliyewahi kufanya kazi Tanzania akiwa na Yanga, kwa sasa ni kocha wa muda wa Chipolopolo, wakati huo pia akiinoa Nchanga Rangers ya Ligi Kuu ya Zambia.

Kampamba amekitaka Chama cha Soka cha Zambia (FAZ) kumpa ajira ya kudumu Lwandamina kuelekea mechi za kuwania tiketi ya fainali zijazo za AFCON za hapo mwakani.

‎Zambia itaanza kusaka tiketi ya AFCON 2027 kwa kuivaa Algeria, mchezo watakaokwenda ugenini mwishoni mwa Septemba, 2026.

‎Kwa mujini wa Kampamba aliyewahi kucheza Nkana na Mamelodi Sundowns, anasema Lwandamina anapaswa kupewa Chipolopolo ili aelekeze nguvu huko, badala ya kujihusisha pia na majukumu ya klabu.

‎“Unajua makocha wa Zambia hawapewi nafasi na mikataba mizuri. Mara nyingi wanafanya kazi kwa kujitolea. Haisaidii kuona Lwandamina akifanya kazi timu ya Taifa na wakati huo huo akiwa na klabu,” amesema.

‎Enzi zake uwanjani, Kampamba aliitumikia Chipolopolo katika fainali za AFCON za mwaka 2002 zilizofanyika nchini Mali.

Kwa upande wake, Lwandamina aliwahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kuanzia mwaka 2015 hadi 2016.

Related articles

Recent articles