24.5 C
New York

Iheanacho aanza na bao Uturuki

Published:

ANKARA, Uturuki

NYOTA wa kimataifa wa Nigeria, Kelechi Iheanacho, amefunga bao katika mechi yake ya kwanza akiwa na Bursaspor ya Ligi Kuu nchini Uturuki.

Katika mchezo wao wa kwanza msimu huu wa Ligi, Bursaspor imezoa pointi tatu za ugenini kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bodrum FK.

Mbali na kufunga, pia Iheanacho aliyewahi kucheza Ligi Kuu ya England akiwa na Leicester City alitoa ‘asisti’ katika bao la pili.

Ni baada ya dakika 90, nyota huyo aliondoka na tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi. “Nimefurahi sana. Mechi za awali huwa ni ngumu. Nimefurahi kuona tumeshinda. Nimefurahi pia kufunga na kutoa asisti,” amesema.

Iheanacho alijiunga na Bursaspor mwezi uliopita (Julai, 2026) akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Celtic ya Ligi Kuu ya Scotland.

Related articles

Recent articles