28.6 C
New York

Ufaransa yatangaza daktari wake kupata Ebola

Published:

PARIS, Ufaransa

MAMLAKA za afya nchini Ufaransa zimetangaza kisa cha kwanza cha maambukizi ya Ebola kwa daktari wake aliyetokea DRC.

Daktari hyo alikuwa DRC katika programu ya Ufaransa kutoa msaada wa kibinadamu katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ya Ufaransa, daktari huyo ameshatengwa katika kituo maalumu cha matibabu ili kuzuia maambukizi zaidi.

DRC ilitangaza mlipuko wa Ebola mwezi Mei, 2026, lakini wataalamu wa afya wamedai kuwa huenda ugonjwa huo ulianza wiki nyingi kabla.

Watu zaidi ya 260 wameripotiwa kupoteza maisha nchini humo, huku wengine 1,000 wakipata maambukizi.

Related articles

Recent articles