19 C
New York

Mabao mawili ya Ronaldo yaweka rekodi tatu

Published:

HOUSTON, Marekani

AMEKASIRIKA! Baada ya kupondwa kwa kiwango alichokionesha katika mchezo wa kwanza dhidi ya DRC, straika wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, amekuja kivingine.

Katika mchezo wa jana Juni 23, 2026, ambao ni wa Kundi K, Ureno iliifunga Uzbekistan mabao 5-0, huku Ronaldo akiingia kambani mara mbili na kuweka rekodi za kutosha.

Kwanza, amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi (miaka 41) baada ya Roger Milla (42) kutikisa nyavu katika mechi za Kombe la Dunia.

Pili, ‘CR7’ ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kufunga bao misimu sita mfululizo ya michuano hiyo ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa).

Tatu, sasa nyota huyo anakuwa ndiye mfungaji bora wa muda wote wa timu ya Taifa ya Ureno, akimpiku mkongwe Eusebio.

Baada ya matokeo hayo, Ureno inaisubiri Colombia katika mchezo wa mwisho, wakati Uzbekistan itamalizana na DRC.

Related articles

Recent articles