NYON, Uswis
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametangaza kuwa Donald Trump atakuwepo uwanjani siku ya fainali ya msimu huu wa Kombe la Dunia.
Katika taarifa yake, pia Infantino ameeleza kuwa Rais huyo wa Marekani ndiye atakayekabidhi kombe kwa timu itakayoshinda siku hiyo.
Fainali ya Kombe la Dunia kwa msimu huu itachezwa Julai 19, 2026, kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey.
Marekani ni moja ya wenyeji watatu, ikishirikiana na Canada na Mexico. “Tutakuwa pamoja na Rais kufurahia fainali na atakabidhi kombe kwa bingwa,” amesema Infantino.
Kati ya mechi 104 za Kombe la Dunia, 78 zinachezwa Marekani lakini Trump hajahudhuria hata moja tangu michuano ilipoanza Juni 11, 2026, kutokana na ugumu wa ratiba zake za kazi.


