Na mwandishi wetu, Gazetini
KOCHA wa Simba, Steve Barker, amesema vijana wake wamejiandaa kimwili na kisaikolojia kukabiliana na Mtibwa Sugar.
Simba wako mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Juni 24, 2026.
Akizungumza na waandishi wa habari, Barker amesema: “Maandalizi kwa upande wetu yapo vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo huu muhimu.”
Wakati huo huo, Barker amesema anafahamu hautokuwa mchezo rahisi kwao lakini wamejipanga kikamilifu kuondoka na pointi tatu za ugenini.
“Tunafahamu tunakwenda kucheza na timu inayopambana kujiweka kwenye mazingira mazuri kwenye msimamo wa Ligi,” amesisitiza.
Simba inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 64, itashuka dimbani ikifahamu kuwa inahitaji pointi mbili tu kuifikia Yanga, ambayo nayo kesho itakuwa dimbani dhidi ya Azam.


