28.6 C
New York

Aliyemtesa mkewe kwa miaka 12 akamatwa

Published:

ISLAMABAD, Pakistan

POLISI nchini Pakistan wanamshikilia mwanaume mmoja kwa kosa la kumtesa mkewe, ikiwamo kumpiga na kumfungia kwenye chumba maalum, akifanya hivyo kwa miaka 12 mfululizo.

Kwa mujibu wa mkewe ambaye ni raia wa Ufaransa, Sylvie Yasmina (54), mumewe alifanya unyama huo pia dhidi ya watoto wao watano.

Familia hiyo inaishi eneo la mbali na mji katika Jimbo la Khyber Pakhtunkhwa na polisi walipofika walikuta Yasmina na watoto wake wakiwa kwenye chumba kilichojificha.

Yasmina aliwaambia polisi kuwa mume wake amewaweka kwenye ‘gereza’ tangu walipohamia Pakistan wakitokea Australia mwaka 2014.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, bibiye huyo na watoto wake wanapatiwa huduma ya kwanza mjini Peshawar, kabla ya kurejeshwa Ufaransa.

Related articles

Recent articles