28.6 C
New York

Shambulizi la Ukraine lakata umeme Crimea

Published:

KYIV, Ukraine

SHAMBULIZI la anga la Ukraine limesababisa sehemu kubwa ya eneo linaloshikiliwa na Urusi nchini humo kukosa huduma ya umeme.

Kwa mujibu wa taarifa, shambulizi hilo la jana Juni 23, 2026, limekata umeme katika Mji Mkuu wa Crimea, Sevastopol.

Kwa upande wake, mamlaka za Ukraine zimethibitisha kushambulia vituo vya uzalishaji wa umeme.

Vikosi vya jeshi la Ukraine vimeendelea kushambulia maeneo wanayoshikilia Urusi, lengo likiwa ni kumlazimisha Rais Vladimir Putin kukubali kukaa mezani ili kumaliza vita.

Katika hatua nyingine, Ukraine imeendelea kuzuia nishati ya mafuta kuingia au kutoka kwenye maeneo yote yaliyo chini ya Urusi.

Related articles

Recent articles