19.2 C
New York

Prodyuza wa Grammy akutwa amefariki

Published:

LOS ANGELES, Marekani

PRODYUZA aliyewahi kuwania tuzo za Grammy, Tay Keith, ameripotiwa kufariki akiwa na umri wa miaka 29.

Tay mkazi wa Nashville alijijengea jina kubwa kwa kufanya kazi na wasanii maarufu, akiwamo Travis Scott, aliyezalisha wimbo wake wa ‘Sicko Mode’.

Wakati huo huo, kwa wasiofahamu, Tay ndiye prodyuza wa ngoma kali ya Drake iitwayo ‘Nonstop’

Kwa mujibu wa polisi wa Nashville, walifika nyumbani kwake na kukuta mshikaji huyo ameshapoteza maisha.

“Hakuna hisia za kuwepo kwa mauaji. Alikutwa amefariki kwenye nyumba yake iliyoeleza iliyoko Mtaa wa Martin. Kifo chake kinaendelea kuchunguzwa,” ilieleza taarifa ya polisi.

Tay aliibuka kwenye tasnia ya muziki mwishoni mwa miaka ya 2010, akifanya kazi pia na Byonce na Eminem.

Related articles

Recent articles