17.4 C
New York

Zungu awakaanga wabunge walioifuata Serengeti Boys

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SPIKA wa Bunge, Mussa Zungu, amewapa siku nne za kujieleza wabunge waliokwenda Morocco kuitazama timu ya soka ya Taifa ya vijana wa U-17, Serengeti Boys, ikicheza fainali ya AFCON dhidi ya Senegal.

Agizo hilo limetolewa leo Juni 4, 2026 na Spika Zungu akisema wabunge hao walisafiri bila kibali chake, hivyo wanapaswa kujieleza.

Katika agizo lake, Spika Zungu amemtaka Katibu wa Bunge kuwaandikia barua mara moja na watoe majibu, vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

“Mawaziri nao wanaondoka wote, najua wana vibali vyao lakini Waziri Mkuu, hawa wasipewe vibali vya ziara wote, akitoka Waziri basi Naibu awepo Bungeni na siyo wanakosekana wote,” amesema Zungu.

Katika hatua nyingine, Spika Zungu ameonya juu ya tabia ya utoro wa vikao kwa baadhi ya wabunge. “Baadhi ya wabunge wanaomba vibali wakisema wanakwenda majimboni lakini wanakwenda nje ya nchi,” amesisitiza.

Related articles

Recent articles