17.4 C
New York

Mke wa Paul wa P-Square afunguka, asema hakufuata pesa

Published:

LAGOS, Nigeria

IVY Ifeoma ambaye ni mke wa pacha wa P-Square, Paul Okoye, amesema hakufuata pesa kwa staa huyo wa muziki.

Ifeoma ameyasema hayo, huku akiwataka wasichana kutokuwa na tamaa ya kuolewa na wanaume matajiri.

Bibiye huyo amedai kuwa alishakuwa tajiri hata kabla ya kukutana na Paul, ambaye kwa sasa jina lake la muziki ni Rudeboy.

“Msinielewe vibaya, kuolewa na tajiri kunaweza kuwa kuzuri, maana kutakupa fursa nyingi. Ninachomaanisha ni kwamba wanawake wapambane wenyewe kuwa matajiri,” amesema.

“Isiwe ndoto ya kila msichana ni kuolewa na tajiri. Kwanini kila mtu awaze kuolewa na tajiri? Mwisho wa siku, ni pesa zake, siyo zako.”

Related articles

Recent articles