MUNICH, Ujerumani
KIWANGO cha umasikini nchini Ujerumani kimeongezeka kwa kasi, ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2020, kwa mujibu wa utafiti wa Taasisi ya Parity Welfare Association.
Katika ripoti ya utafiti huo, watu milioni 13.34, sawa na asilimia 16.1 ya raia wote wa Ujerumani walikuwa kwenye umasikini mwaka 2025.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Ujerumani, idadi hiyo ni kubwa, ikilinganishwa na asilimia 15.5 mwaka wa nyuma yake, 2024.
Utafiti wa sasa umeainisha kuwa wazazi wanaolea watoto bila wenza ni waathirika wakubwa wa umasikini, kama ilivyo kwa watu wanaoishi peke yao.
Wakati huo huo, utafiti imebaini kuwa kiwango cha umasikini ni kikubwa zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 na wazee wa miaka zaidi ya 65.
Pia, kiwango cha umasikini kimetofautiana kutoka eneo moja na ni jingine. Kwamba hali ni mbaya zaidi Saxony-Anhalt na Bremen, ikilinganishwa na Bavaria na Baden-Württemberg.
Kwa vigezo vya Umoja wa Mataifa (EU), watu wanaotajwa kuwa masikini ni wale kipato chao ni chini ya asilimia 60 ya Pato la Taifa.


