10.9 C
New York

Israel kumpokea Kanye West?

Published:

LOS ANGELES, Marekani

RAPA asiyeishiwa matukio, Kanye West, anaendelea na ziara yake ya muziki katika maeneo mbalimbali duniani na sasa amepanga kuibukia Israel.

Kanye anaendeleza ziara ya kuwaomba radhi mashabiki kwa kauli za kibaguzi alizowahi kutoa dhidi ya wayahudi miaka michache iliyopita.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, tayari supastaa huyo ameanza kuwasiliana na waratibu wa shoo nchini Israel ili kuona uwezekano wa kwenda huko.

Hata hivyo, wengi wanatilia shaka uwezekano wa shoo hiyo kufanyika, ikihofiwa kuwa huenda mamlaka za Israel zikamzuia kuingia nchini humo, kama ilivyotokea Uingereza.

Mara ya mwisho kwa Kanye kutumbuiza Israel ilikuwa mwaka 2015, miezi michache tu baada ya kufika nchini humo kwa matembezi akiwa na mpenzi wake wa wakati huo, Kim Kardashian.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img