23.1 C
New York

Jay-Z alikwepa ‘bifu’ la Drake, Lamar

Published:

LOS ANGELES, Marekani

LEJENDARI wa muziki wa Hip hop, Jay-Z, amesema hana upande katika bifu linaloendelea kati ya marapa Drake na Kendrick Lamar.

Kwa kauli hiyo, Jay-Z ni kama amekanusha kile kilichoelezwa awali, kamba yeye ni upande wa Drake.

Jay-Z, ambaye ni mume wa bibiye maarufu kwenye muziki, Beyonce Knowles, ameenda mbali zaidi kuhusu bifu la wasanii wenzake hao.

Akizungumzia hilo, amedai kuwa haoni kama muziki wa Hip hop unahitaji bifu kwa sasa.

Aidha, mkongwe huyo amesema uwepo wa bifu unachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha soko la muziki wa Hip hop.

Kwa upande mwingine, bosi huyo wa lebo maarufu ya Roc Nation amesema muziki wa Hip hop utapata mafanikio makubwa zaidi endapo wasanii wataacha kuonana maadui.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img