Na mwandishi wetu, Gazetini
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi.
Taarifa kwa umma kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka, imeeleza kuwa Lukuvi amefariki leo Jumatano, Machi 25, 2026 kutokana na ugonjwa wa mshituko wa moyo.
Ikaeleza pia, Lukuvi aliyezaliwa Agosti 15, 1955 amekutwa na umauti akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
“Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo,” amesema Dk. Kusiluka.
Ikumbukwe, Lukuvi amekuwa mmoja ya wabunge wa mufa mrefu, akiwa mwakilishi wa Jimbo la Ismani tangu mwaka 1995.


