13.5 C
New York

Kofi Olomide aaga ukapera, amuoa Cindy

Published:

KINSHASA, DRC

BAADA ya miaka 20 ya kuwa kwenye mahusiano, hatimaye lejendari wa muziki nchini DRC, Koffi Olomide, amefunga ndoa na Cindy Le Coeur

Koffi ana umri wa miaka 69, ikimaanisha kwamba amemzidi miaka 23 mke wake huyo ambaye pia ni mwanamuziki.

Kupitia akaunti zake za mtandao ya kijamii, Mfalme huyo wa Ndombolo ameposti picha na video za sherehe ya harusi yao ya kifahari.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na binti wa Koffi, Minou Olomide, ambaye alikuwa mstari wa mbele kumsapoti mzee wake huyo.

Baada ya kuposti video na picha, wafuasi wake huko mitandaoni walimpongeza na wengine kushangazwa na namna Koffi na Cindy walivyodumu kwenye uchumba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img