8 C
New York

Britney Spears sasa siyo mmiliki wa kazi zake

Published:

LOS ANGELES, Marekani

BIBIYE mwenye jina na mafanikio makubwa katika muziki wa Pop duniani, Britney Spears, kwa sasa hamiliki haki zozote za kazi alizofanya baada ya uamuzi wake wa kuziuza.

Kwa mujibu wa kile kinachoelezwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), nyota huyo mwenye umri wa miaka 44 ameuza haki za muziki wake kwa Kampuni ya Primary Wave.

BBC wameeleza kuwa Britney akichukua uamuzi huo Desemba 30, 2025 na alivuna kitita cha Dola za Marekani milioni 200.

Katika maisha yake ya muziki, alijizolea umaarufu mkubwa kupitia ngoma zake zilizofanya vizuri, zikiwamo ‘Baby One More Time’, ‘I Did It Again’, ‘Toxic’ na ‘Gimme More’.

Hata hivyo, Britney aliwashangaza wengi Januari, 2024, alipotangaza kuwa hatorejea kwenye soko la muziki. Aliachia wimbo wake wa mwisho mwaka 2022, ambao akishirikiana na Elton John.

Britney si mwamuzi wa kwanza kuuza haki zote za kazi zake. Bruce Springsteen, Justin Bieber, Justin Timberlake na Shakira waliwahi kufanya hivyo kwa nyakati tofauti.

Springsteen aliiuzia Sony mwaka 2021 na kuvuna Dola milioni 500, wakati Bieber alipata Dola milioni 200 alipofanya biashara hiyo na Kampuni ya Hipgnosis Songs Capital mwaka 2023.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img