6.4 C
New York

Maria Carey kutumbuiza Olimpiki

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MWANAMUZIKI ambaye pia ni mshindi mara tano wa tuzo za Grammy, Mariah Carey, atakuwa miongoni mwa watumbuizaji wakati wa hafla ya ufunguzi wa michuano ya Olimpiki hapo mwakani.

Michuano hiyo itaanza Februari 6-22 na hafla ya ufunguzi itafanyika katika Uwanja wa San Siro mjini Milan, Italia.

Carey mwenye umri wa miaka 56, hii si mara yake ya kwanza kualikwa kutumbuiza katika matukio ya michezo.

Itakumbukwa, raia huyo wa Marekani alitumbuiza katika mechi za Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA) mwaka 2003.

Pia, Carey alialikwa kufanya kazi hiyo wakati wa mechi ya fainali ya michuano mikubwa ya tenesi ya US Open mwaka 2020.

Kwa kuingia Olimpiki, sasa Carey anaingia kwenye historia ya kushiriki michuano hiyo, akifuata nyayo za Celine Dion and Lady Gaga.

Celine na Gaga walishiriki kwa pamoja kufanya ‘shoo’ wakati wa sherehe za ufunguzi wa michuano ya Olimpiki iliyopita ya mwaka jana jijini Paris, Ufaransa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img