13.1 C
New York

Usiyoyajua kuhusu Mapinduzi Cup 2026

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

MSIMU huu wa Kombe la Mapinduzi umekuja na sura mpya, kubwa ikiwa ni ongezeko la Shilingi milioni 50 katika zawadi ya timu itakayotwaa ubingwa.

Tofauti na msimu uliopita, ambapo bingwa alilamba Shilingi milioni 100, safari hii atajiondokea na Shilingi milioni 150.

Aidha, mshindi wa pili katika mashindano hayo atajizolea milioni 100 alizopata bingwa wa msimu uliopita, ambapo alilamba milioni 70.

Msimu uliopita, zilishiriki timu za taifa baada ya klabu kama ilivyozoeleka, ambapo wenyeji Zanzibar Heroes walibakiza Kombe kwa kuifunga Burkina Faso mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.

Safari hii, klabu nane zitatoana jasho, soka la Zanzibar likitarajiwa kuwakilishwa na Mlandege, Fufuni na KVZ.
Kwa upande wa Bara, ni Yanga, Simba, Azam na Singida Black Stars. Pia, URA ya Uganda itashiriki kama ‘mgeni mwalikwa’ nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wachezaji watangaziwa fungu

Kwa mujibu wa ratiba, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Desemba 28, mwaka huu, na ukomo wake ni Januari 13, mwakani.

Dimba la Amaan.

Kwa kila mechi ya hatua ya makundi, mchezaji atakayeibuka nyota wa mchezo atalamba kitita cha Shilingi milioni moja. Zawadi hiyo itaongezeka hadi milioni 2 kwa mechi za robo fainali na milioni 3 kwa fainali.

Azam kuendeleza ubabe?

Historia iko hivi; tangu michuano hiyo ilipoanza kuhusisha timu za nje ya Zanzibar mwaka 2007, Azam ndiyo iliyotwaa ubingwa mara nyingi (5).

Matajiri hao wa Chamazi, Temeke jijini Dar es Salaam, ni mabingwa wa michuano hiyo kwa miaka ya 2012, 2013, 2017, 2018 na 2019).

Hivyo, Azam watakwenda kwenye mashindano wakiwa na ukame wa kulikosa taji hilo kwa miaka takribani sita.
Simba ‘Wekundu wa Msimbazi’ wanashika nafasi ya pili wakiwa na mataji manne (2008, 2011, 2015 na 2022), wakati wapinzani wao wakubwa, Yanga, wakiwa wamefanya hivyo mara mbili (2007 na 2021).

Timu zingine zilizowahi kuwa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi ni Mlandege (2023-2024), Mtibwa Sugar (2010 na 2020), Miembeni (2009), KCCA (2014), URA (2016) na Zanzibar Heroes (2025).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img