25.2 C
New York

Nyota sita Argentina kupigwa ‘stop’ Kombe la Dunia

Published:

NYON, Uswis

WACHEZAJI wapatao sita wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina huenda wakafungiwa kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia za mwaka 2030.

Kwa mujibu wa Gazeti la Sun, nyota walio hatarini kushukiwa na rungu hilo ni Nahuel Molina, Leandro Paredes, Thiago Almada, Cristian Romero, Lisandro Martinez na Giovani Lo Celso.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linaichunguza Argentina kwa makosa kadhaa, zikiwamo vurugu zilizojitokeza siku ya fainali ya msimu huu wa Kombe la Dunia dhidi ya Hispania.

Argentina ilipoteza mchezo huo kwa kipigo cha bao 1-0 lakini wachezaji wake hao walijiingiza katika vitendo vya utovu wa nidhamu dhidi ya wenzao wa Hispania.

Kamera za uwanjani zilimnasa Molina akigombana na kiungo Rodri, kabla ya tukio jingine la Paredes kuwashambulia Eric Garcia na Gavi.

Mbali na matukio hayo, Romero, Martinez na Lo Celso nao wanachunguza kwa kitendo chao cha kuonesha bango lililobeba ujumbe wa kisiasa.

Ujumbe huo ulilenga uadui wa kisiasa uliopo kati ya Argentina na Uingereza, mataifa ambayo yamekuwa yakigombea Visiwa vya Falkland vilivyoko Kusini mwa Atlantic.

Related articles

Recent articles