20.7 C
New York

Howe kuachia benchi Newcastle

Published:

LONDON, Uingereza

HUENDA kocha wa Newcastle United, Eddie Howe, akaachia ngazi katika benchi la ufundi la timu hiyo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari maarufu, David Ornstein.

Kwa mujibu wa Ornstein, tayari kocha huyo wa kimataifa wa England ameshawaambia mabosi wa Newcastle United kuwa anataka kuondoka.

Ikiwa ni miaka mitano aliyofanya kazi, taarifa zinaeleza kuwa Matthias Jaissle anayefanya kazi na Al Ahli ya Saudi Arabia.

Taarifa za Howe kuondoka zinakuja zikiwa ni siku 25 tu zimebaki kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya England.

Newcastle watatupa karata yao ya kwanza msimu huo wa 2026-27 kwa kuikaribisha Liverpool.

Msimu uliopita, Newcastle United ilimaliza katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Related articles

Recent articles