21.6 C
New York

Penzi la ujana hadi ndoa; kapo za mastaa zilizodumu miaka mingi

Published:

LOS ANGELES, Marekani

KUDUMU muda mrefu kwenye mahusiano ya kimapenzi au hata ndoa si jambo rahisi, hasa unapokuwa na jina na mafanikio makubwa. Mastaa wengi wameshindwa.

Hata hivyo, wapo baadhi ya mastaa walioweza kukwepa vishawishi vyote na kuamua kubaki na wapenzi wao wa muda mrefu. Tangu wakiwa shule.

LEBRON JAMES & SAVANNAH

Staa wa Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani (NBA), ambaye amekuwa na bibiye Savannah tangu walipofahamiana wakiwa sekondari, ingawa walisoma shule tofauti.

LeBron na Savannah walifunga ndoa Sptemba 14, 2013. Wawili hao wana watoto watatu; Bronny aliyezaliwa mwaka 2004, Bryce (2007) na Zhuri (2014).

SNOOP DOGG & BROADUS

Walikutana wakiwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Long Beach Polytechnic. Snoop na bibiye Broadus walifunga ndoa mwaka 1997 na sasa wana watoto watatu, ingawa Snoop mmoja katika uhusiano wake na Laurie Helmond.

Akifichua siri ya kudumu kwa penzi na ndoa yao, Snoop aliwahi kusema: “Nafikiri ni kwa sababu tulikutana tukiwa vijana, kila mmoja akaamua kujitoa kwa ajili ya mwenzake. Alijuwa ndoto zangu, nikajuwa na zake.”

LL Cool J & SMITH

Mwanamuziki LL Cool J alifahamiana na bibiye Simone I. Smith wakiwa vijana Aliyewakutanisha ni mmoja ya ndugu wa Smith. Hiyo ilikuwa mwaka 1987.

Ilipofika mwaka 1995, walifunga ndoa na sasa wana watoto wao wanne. “Ndoa siyo kwa watu dhaifu, inahitaji uaminifu,” alisema Smith akizungumzia kudumu kwao kwa muda mrefu.

Related articles

Recent articles