22.4 C
New York

Davido kuibukia uigizaji wa ‘muvi’

Published:

LAGOS, Nigeria

SUPASTAA wa muziki wa Afrobeats, Davido, ameeleza nia yake ya kuwa mwigizaji kwenye soko la filamu nchini Nigeria (Nollywood).

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Davido amesema tayari ameshaandaa filamu mbili kama prodyuza lakini sasa anataka kuwa mwigizaji.

Aidha, mwanamuziki huyo amefichua kuwa tayari amerekodi filamu ambayo itaingia sokoni hivi karibuni.

“Nataka kuingia moja kwa moja kwenye filamu. Nataka kuanza kuigiza. Nataka kuwa mwigizaji katika siku za usoni,” amesema Davido.

Katika hatua nyingine, staa huyo ameweka wazi kuwa muziki unabadilika, hivyo ni bora wasanii wakafahamu hilo na kujiongeza.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa hana mpango na wala hafikirii kuachana na muziki kwani ndiyo kazi anayoipenda zaidi.

Related articles

Recent articles